Sekta ya Usafiri ya Kenya yafufuka polepole kutokana na kuwapatia chanjo wananchi wake
2021-08-24 10:06:26| CRI

Sekta ya Usafiri ya Kenya yafufuka polepole kutokana na kuwapatia chanjo wananchi wake_fororder_1

Sekta ya usafiri na huduma ya Kenya imeanza kufufuka polepole wakati ambapo nchi inaendelea na zoezi la kuchanja watu dhidi ya UVIKO-19 huku ikivutia wageni kutoka masoko mapya.

Joseph Boinnet, katibu tawala wa Wizara ya Utalii na Wanyamapori, amesema serikali imeweka kipaumbele katika kuongeza hatua za kupambana na virusi na mambo anuai ili kuhimiza watalii wafike nchini. Amesema hatua makini zinachukuliwa na serikali zikiwemo kufungua tena hifadhi za usimamizi wa wanyamapori za umma na binafsi ambazo zimerahisisha kufufuka kwa sekta ya huduma.

Takwimu kutoka Taasisi ya Utafiti wa Utalii zinaonesha kuwa sekta hiyo imepoteza ajira milioni 1.2 kutokana na athari za janga la Corona, ambazo ni sawa na hasara ya Shilingi bilioni 192 za Kenya kutoka mapato ya moja kwa moja ya kazi, na dola bilioni 4.48 kwa thamani ya sekta nzima ya utalii.