China yaahidi kuendelea na juhudi za kuchangia amani na maendeleo ya Pembe ya Afrika
2021-08-24 10:05:24| CRI

Naibu balozi wa China kwenye Umoja wa Mataifa Dai Bing amesema China inafuatilia kwa makini hali ya Pembe ya Afrika na kutarajia nchi za kanda hiyo kudumisha amani na utulivu, kutimiza maendeleo na ustawi, na kuunga mkono Umoja wa Afrika na nchi kutatua masuala yao kwa njia zao.

Balozi Dai alisema hayo alipozungumza kwa njia ya video na mjumbe maalum wa katibu mkuu wa Umoja huo kuhusu Pembe ya Afrika Bw. Parfait Onanga-Anyanga. Balozi Dai pia ametoa wito kwa Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika kuongeza uratibu na kufanya kazi za kiujenzi ili kuhimiza utatuzi wa masuala yanayofuatiliwa. Ameongeza kuwa China imetoa misaada ya dharura ya chakula na chanjo dhidi ya virusi vya Corona kwa nchi za Pembe ya Afrika.

Bw. Onanga ameishukuru China kwa kuonesha ushawishi wake katika Pembe ya Afrika na kutarajia kuendelea na juhudi zake za kuboresha hali ya kanda hiyo.