Jumuiya ya Afrika Mashariki yapitisha mpango wa kuanzisha jukwaa la amani na usalama kwa vijana
2021-08-24 10:03:12| CRI

Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) imesema imepitisha mpango wa kuanzisha jukwaa la kikanda la amani na usalama kwa vijana, ili kuwafanya vijana hao washiriki zaidi kwenye mambo ya usalama ya kikanda.

Kwenye taarifa yake iliyotolewa jana na makao makuu yake mjini Arusha, EAC imesema mpango huo ulipitishwa Ijumaa iliyopita kwenye mkutano wa baraza la pamoja la EAC linaloshughulikia mambo ya ulinzi, usalama kati ya nchi na sera za kidiplomasia. Baraza hilo limeelekeza sekretarieti na nchi wanachama watunge mkakati wa mawasiliano ya amani na usalama, ili kutoa uelewa juu ya mfumo wa sasa wa amani na usalama, na kuwahamasisha vijana wa ngazi mbalimbali washiriki kwenye mpango huo.

Baraza hilo limetoa wito wa kuanzisha mfumo wa kutambua maeneo yenye uwezekano wa kutokuwa na usalama, ambayo yanahitaji vijana kushughulikia.