Rwanda yapanua utoaji wa chanjo za Corona kwa watu wanaofaa
2021-08-24 10:04:01| CRI

Wizara ya Afya ya Rwanda imesema awamu ya tatu ya kuwapatia chanjo za Corona wananchi wenye umri wa miaka 18 na zaidi imeanzishwa jana mjini Kigali, ambapo kuna wagonjwa wengi zaidi waliothibitishwa kuambukizwa nchini humo.

Waziri wa nchi wa Rwanda anayeshughulikia mambo ya afya Tharcisse Mpunga amesema, wizara ya afya inataka asilimia zaidi ya 90 ya watu wanaofaa kupata chanjo washiriki kwenye zoezi hilo la wiki mbili kwenye maeneo mbalimbali ya wilaya ya Kigali, ikiwa ni pamoja na Gasabo, Kicukiro na Nyarugenge.

Ameongeza kuwa wamepanua watu wanaofaa kupatiwa chanjo kwa ajili ya kuwapatia chanjo wafanyakazi kwenye sekta mbalimbali ili kurejesha hali ya kawaida ya biashara nchini humo. Aidha, watumishi wa afya watawafuata nyumbani wazee na wale wenye tatizo la kutembea ili kuwapatia chanjo.