Jamhuri ya Kongo yachukua uenyekiti wa zamu wa OPEC kwa mwaka 2022
2021-08-24 10:04:47| CRI

Katibu mkuu wa Shirika la Nchi zinazosafirisha Petroli (OPEC) Bw. Mohammed Barkindo amesema Jamhuri ya Kongo itaipokea Angola na kuwa nchi mwenyikiti wa zamu wa OPEC wa mwaka 2022.

Bw. Barkindo amesema hayo baada ya kuzungumza na waziri mkuu wa Jamhuri ya Kongo Anatole Collinet Makosso, wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku tatu huko Brazzaville, mji mkuu wa Kongo. Aidha amesema waziri mkuu pia alizihakikishia nchi wanachama na zisizo wanachama kuziunga mkono.

Jamhuri ya Kongo ni nchi ya tatu inayoongoza kwa uzalishaji wa mafuta Kusini mwa Jangwa la Sahara baada ya Nigeria na Angola, ikizalisha mapipa 336,000 ya mafuta ghafi kwa wastani kila siku.