Rais Xi Jinping wa China akagua Misitu ya Saihanba
2021-08-24 11:00:02| CRI

Rais Xi Jinping wa China akagua Misitu ya Saihanba_fororder___172.100.100.3_temp_9500032_1_9500032_1_1_a609e6d4-737f-4117-8ef0-4813f9362817

Rais Xi Jinping wa China amekagua Misitu ya Saihanba mkoani Hebei, akichunguza mazingira ya asili na hali ya ukuaji wa misitu, na kusikiliza ripoti kuhusu kazi za usimamizi wa mazingira, misitu, mashamba, maziwa, na mfumo wa udongo na mchanga mkoani Hebei, na kuwatembelea walinzi wa Misitu ya Saihanba.

Eneo la Saihanba lilikuwa jangwa lisilo na majani. Mwaka 1962 China iliamua kupanda misitu katika eneo hilo. Baada ya miaka 59, Saihanba imekuwa sehemu yenye misitu mikubwa zaidi iliyopandwa na binadamu duniani.