Huawei yazindua nishati safi ya jua kwa kaya za Wakenya
2021-08-25 10:00:05| CRI

Huawei yazindua nishati safi ya jua kwa kaya za Wakenya_fororder_1

Kampuni ya mawasiliano ya simu ya China Huawei imezindua suluhisho la nishati ya jua jumuishi kwa kaya za Wakenya, kufuatia wito wa kuhamasisha matumizi machache ya caboni nchini.

Kwenye taarifa yake aliyoitoa mjini Nairobi, Mkurugenzi Mkuu wa Huawei ya Kenya Will Meng amesema uzinduzi huo wa LUNA 2000, utahakikisha kwamba maeneo ya wakazi yanapata nishati ya umeme safi na watakayomudu. Kwa mujibu wa Meng, Huawei itatumia uzoefu wake na utaalamu wake mkubwa katika kuendeleza nishati ya kisasa ya umeme ili kuwawezesha Wakenya na maeneo ya biashara kupunguza matumizi ya caboni.

Naye katibu mkuu wa Wizara ya Nishati Joseph Njoroge amesema uzinduzi wa LUNA 2000 wa Huawei utahakikisha kwamba nyumba zina nishati salama ambayo ni muhimu kwa vifaa vya umeme na internet katika wakati ambao kufanya kazi za ofisini nyumbani limekuwa ni jambo la kawaida.