Ofisa wa China asisitiza mawasiliano ya kimkakati katika ushirikiano wa BRICS
2021-08-25 10:02:36| CRI

Ofisa mwandamizi wa China asisitiza mawasiliano ya kimkakati katika ushirikiano wa BRICS_fororder_2

Nchi za BRICS zinatakiwa kuwasiliana zaidi kimkakati, kuongeza hali ya kuaminiana kisiasa, kuimarisha uratibu kwenye masuala ya usalama na kufanya maandalizi yote kwa ajili ya Mkutano wa 13 wa Wakuu wa BRICS.

Hayo yamesemwa na Yang Jiechi, mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China CPC kwenye Mkutano wa 11 wa Wawakilishi wa Ngazi ya Juu wa BRICS kuhusu Masuala ya Usalama uliofanyika jana kwa njia ya video. Amesisitiza kuwa nchi za BRICS zinatakiwa kufuata miongozo ya pamoja ya wakuu wa nchi hizi tano na kushikilia moyo wa BRICS wa uwazi, ujumuishi na ushirikiano wa kutafuta mafaniko ya pamoja.

Yang ameongeza kuwa nchi za BRICS pia zinatakiwa kushirikiana pamoja ili kukabiliana na changamoto na matishio ya kiusalama, kuungana pamoja kupambana na janga la COVID-19 na kufuata sayansi badala ya madhumuni ya siasa katika juhudi za kutafuta chanzo cha virusi.