Mawaziri wa afya wa Afrika waahidi kuchukua hatua zaidi za pamoja dhidi ya UVIKO-19
2021-08-25 10:01:07| CRI

Mawaziri wa afya wa Afrika waahidi kuchukua hatua zaidi za pamoja dhidi ya UVIKO-19_fororder_3

Mawaziri wa afya wa nchi za Afrika zilizo kusini mwa Sahara wameahidi kuimarisha mapambano dhidi ya UVIKO-19 kupitia kuongeza kutoa chanjo na kupeana maarifa ya kitaalamu.

Wakiongea kwenye kikao cha 71 cha Kamati ya Kikanda ya Afrika katika Shirika la Afya Duniani (WHO), mawaziri hao wamesema kudhibiti janga la Corona ndio ufunguo wa kufufua uchumi wa Afrika. Waziri wa afya wa Cote d’lvoire Pierre Ng’ou Dimba amesema Afrika bado inaweza kuepuka athari mbaya za janga la Corona, kwa kuongeza kuchanja watu, kurekebisha vituo vya huduma za afya na kufuata hatua za kuzuia virusi. Amesisitiza kuwa utafiti wa pamoja, kuongeza ufuatiliaji, kupima na kupata huduma kwa wakati, vitu hivi vitaimarisha uwezo wa nchi za Afrika katika kukabiliana na janga.

Zaidi ya wajumbe 400 wakiwemo mawaziri wa afya, wawakilishi wa vyombo mbalimbali, wasomi na asasi za kiraia wameshiriki kwenye mkutano huo uliofanyika kwa njia ya video.