Algeria yasitisha uhusiano wa kidiplomasia na Morocco
2021-08-25 09:57:49| CRI

Waziri wa mambo ya nje wa Algeria Bw. Ramtane Lamamra jana alitangaza kwamba Algeria itasitisha uhusiano wa kidiplomasia na Morocco kuanzia Jumanne.

Akisoma barua kwa niaba ya rais Abdelmadjid Tebboune wa Algeria kwenye mkutano na wanahabari uliofanyika katika Kituo cha mikutano ya kimataifa mjini Algiers, Lamamra amesema uamuzi huo unatokana na sera ya upande mmoja inayochukuliwa na Morocco kwa muda mrefu. Lamamra amekumbusha vitendo cha upinzani vya Morocco dhidi ya Algeria tangu katikati ya mwezi Julai, hasa uungaji mkono anaopewa ambao balozi wa Morocco kwenye Umoja wa Mataifa anauita ni haki ya kundi la uamuzi binafsi wa watu wa “Kabyle” nchini Nigeria. Pia ameituhumu Morocco kwa kuyaunga mkono makundi mawili ambayo Algeria yanayachukulia kuwa ni ya kigaidi, pamoja na “Opresheni ya ujasusi ya Pegasus” inayoshirikiwa na Morocco.