China yasema wito wake wa kuchunguza Fort Detrick unaeleweka na wa haki
2021-08-27 10:06:00| CRI

China yasema wito wake wa kuchunguza Fort Detrick unaeleweka na wa haki_fororder_3

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Wang Wenbin amesema China inatoa wito wa kuchunguza maabara ya Fort Detrick ya Marekani na Chuo Kikuu cha Carolina Kaskazini (UNC) kwa ajili ya kuondokana na usumbufu unaotokana na kitendo cha Marekani kufanya suala la utafutaji wa chanzo cha virusi vya Corona kuwa la kisiasa na kuandaa mazingira mazuri kwa ajili ya utafiti wa kisayansi, ambapo amesisitiza kuwa wito huo unaeleweka na wa haki.

Wang amesema hayo kwenye mkutano na wanahabari wakati alipojibu swali kuwa kwa nini China inapinga vikali dai la virusi kuvuja kutoka kwenye maabara, lakini wakati huohuo inataka ufanyike uchunguzi kwenye Fort Detrick. Ameeleza kuwa wataalam wa China na wa Shirika la Afya Duniani WHO wametoa hitimisho kuwa haiwezekani kabisa kwa virusi kutoka kwenye maabara ya Wuhan. Wataalam kote duniani wakiwemo wale wanaoishi nchini Marekani pia wanaamini kuwa hakuna ushahidi unaounga mkono dai hilo. Lakini ni Marekani inayopinga hitimisho hilo la kisayansi na kusisitiza kuwa virusi vilitoka kwenye maabara ya Wuhan.

Ameongeza kuwa kwa vile maabara ya Wuhan imetembelewa na wataalam wa WHO mara mbili na maabara ya Fort Detrick na UNC yenye historia ndefu ya utafiti wa virusi vya Corona pamoja na kumbukumbu mbaya za usalama, kama Marekani inashikilia nadharia ya virusi kutoka kwenye maabara, basi Marekani inapaswa kufungua Fort Detrick kwa ajili ya uchunguzi wa kimataifa. Vilevile kama sekretarieti ya WHO inaona uwezekano wa virusi kutoka kwenye maabara hauwezi kufutwa, pia inapaswa kuchunguza Fort Detrick.