Uwekezaji wa moja kwa moja wa viwanda vya China barani Afrika wazidi dola za kimarekani bilioni 56
2021-08-27 10:04:35| CRI

Uwekezaji wa moja kwa moja wa viwanda vya China barani Afrika wazidi dola za kimarekani bilioni 56_fororder_2

Ripoti kuhusu uwekezaji wa viwanda vya China barani Afrika iliyotolewa kwa kiingereza na kifaransa imetangazwa jana hapa Beijing.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo iliyoandaliwa na Chama cha umma cha wafanyabiashara kati ya China na Afrika, hadi kufikia mwishoni mwa mwaka 2020, uwekezaji wa moja kwa moja wa viwanda vya China barani Afrika umezidi dola za kimarekani bilioni 56, na viwanda vya watu binafsi vya China vimekuwa nguzo ya uwekezaji wa moja kwa moja barani Afrika.

Ripoti hiyo imeonesha kuwa, ongezeko la uwekezaji wa viwanda vya China linahusisha nchi 47 barani Afrika, na kuchangia utandawazi wa viwanda na kuboresha maisha ya watu barani humo. Tokea mwaka 2007, miradi ya ujenzi ya China inachukua theluthi mbili ya zana za miundombinu iliyojengwa upya barani Afrika; asilimia 50 ya viwanda vya watu binafsi vya China vimeingiza bidhaa na huduma mpya katika masoko ya Afrika na ajira kwa wafanyakazi wa Afrika wa viwanda hivyo vya China zimefikia asilimia 89.

Katibu mkuu wa Eneo la biashara huria la Afrika lililozinduliwa tarehe 1 Januari mwaka huu, Wamkele Mene, amesema eneo hilo limetoa jukwaa moja litakalowezesha viwanda na wawekezaji kuonesha umuhimu mkubwa zaidi katika maendeleo ya uchumi barani Afrika.