Zanzibar yaeleza wasiwasi kuhusu kasi ndogo ya utoaji chanjo ya COVID-19
2021-08-30 08:48:48| CRI

Mamlaka visiwani Zanzibar, Tanzania jana zimeeleza wasiwasi kutokana na kile wanachokiita kama “kasi ndogo” ya zoezi ya utoaji chanjo ya COVID-19.

Mkurugenzi mkuu katika Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto Bw. Abdallah Suleiman Ali alisema ni watu 10,866 tu ndio waliopewa chanjo hadi kufikia Agosti 24, ikilinganishwa na dozi 85,000 zilizopokelewa mwezi Juni na Julai.

Zanzibar ilizindua kampeni ya utoaji chanjo ya COVID-19 Julai 22, na ilipokea shehena ya chanjo ya Sinovac iliyotolewa na China Julai 31. Kwa mujibu wa Wizara ya Afya ya Zanzibar, hadi kufikia Jumamosi idadi ya watu walioambukizwa virusi vya Corona iliongezeka hadi 876 kutoka 390 ya Agosti 10, huku idadi ya vifo ikifikia 40 kutoka 15 iliyorekodiwa Agosti 10.