Polisi wa Tanzania wawakamata pembe za ndovu na majangili 9 waliokuwa na silaha
2021-08-31 09:34:28| CRI

 

-Polisi wa Tanzania wamesema wamekamata pembe tatu za ndovu zenye uzito wa kilo 24.72 pamoja na watu tisa wanaoshukiwa kuwa majangili wenye silaha.

Mkuu wa polisi mkoa wa Katavi Bw. Benjamin Kuzaga, amesema katika operesheni maalum iliyofanywa wiki iliyopita na polisi na walinzi wa wanyamapori, washukiwa hao tisa walikamatwa kwenye mbuga ya taifa ya Katavi wakiwa na bunduki na raundi 28 za risasi.