Kenya kukusanya dola za Kimarekani laki 9.1 kwa ajili ya uhifadhi wa tembo
2021-08-31 09:34:57| CRI

Waziri wa utalii na wanyamapori wa Kenya Bwana Najib Balala  amesema Kenya ina mpango wa kukusanya dola za kimarekani laki 9.1 kwa ajili ya uhifadhi wa tembo.

Bwana Balala amesema fedha hizo zitakusanywa wakati wa Tamasha la kwanza la kuwapa majina Tembo la Magical Kenya, na zitatumika kusaidia mipango ya uhifadhi na kuongeza idadi ya Tembo katika mbuga za wanyama za taifa na maeneo ya hifadhi ya wanyama.

Uzinduzi wa tamasha hilo unatarajiwa kufanyika tarehe 8 Oktoba mjini Nairobi. Watu wataruhusiwa kuwapatia majina Tembo waliochaguliwa baada ya kuchangia pesa kwenye mpango huo, wenye lengo la kuongeza juhudi za uhifadhi wa wanyama walio hatarini kutoweka.