Wizara ya mambo ya nje ya China yasema ushirikiano wa uwekezaji kati ya China na Afrika una mustakabali mzuri
2021-08-31 09:22:22| CRI

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Wang Wenbin, amesema serikali ya China siku zote inatia moyo kampuni kushiriki kwenye mikakati ya maendeleo ya Afrika, kutoa mchango katika kuzisaidia nchi za Afrika kutimiza maendeleo endelevu, huku ikiwa na imani kuwa ushirikiano wa uwekezaji kati ya China na Afrika una mustakabali mzuri na uwezo mkubwa.

Bw. Wang amesema ripoti kuhusu kampuni za China kuwekeza barani Afrika imepongezwa na watu kutoka jamii mbalimbali, ambao wengi wanaona kuwa uwekezaji wa kampuni za China barani Afrika unanufanisha pande mbili, na kuendana na mahitaji ya maendeleo ya Afrika, na ushirikiano wa uwekezaji kati ya China na Afrika wenye sifa ya juu una mustakabali mzuri zaidi.

Pia amesema serikali ya China inazitia moyo kampuni za China kushiriki kwenye mikakati ya maendeleo ya Afrika, kujiunga na jamii za huko, kutekeleza wajibu wa kijamii, kuwanufaisha wakazi wa huko na kutoa mchango katika maendeleo endelevu ya nchi za Afrika.