Viongozi wa Taliban wakutana kujadili uundwaji serikali mpya
2021-09-01 10:39:32| CRI

Msemaji wa Taliban nchini Afghanistan Zabiullah Mujahid amesema wameitisha mkutano wa viongozi kujadili uundwaji wa serikali mpya huko mkoa wa Kandahar, kusini mwa nchi hiyo. Katika mkutano huo uliongozwa na kiongozi mkuu wa Taliban Hibatullah Akhundzada kuanzia tarehe 28 hadi tarehe 30 Agosti, masuala mbalimbali ya kisiasa, kiusalama na kijamii yalijadiliwa.

Bw. Mujahid amesema wafanyabiashara na wawekezaji wa Afghanistan wanatakiwa kushiriki kwenye utatuzi wa changamoto za kiuchumi. Na nchi hiyo inapendelea kuendeleza mahusiano ya kiuchumi na nchi mbalimbali duniani ikiwa ni pamoja na Marekani, huku akitarajia nchi zote zidumishe uhusiano mzuri wa kisiasa na kibiashara na Afghanistan.