Katibu Mkuu wa UM ataka kukomeshwa kwa ubaguzi wa rangi kwenye siku ya kimataifa ya watu wenye asili ya Afrika
2021-09-01 08:58:17| CRI

Katibu Mkuu wa UM ataka kukomeshwa kwa ubaguzi wa rangi kwenye siku ya kimataifa ya watu wenye asili ya Afrika_fororder_VCG111345995048

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres ametoa mwito wa kukomesha ubaguzi wa rangi, ametoa mwito huo wakati wa maadhimisho ya siku ya kwanza ya kimataifa ya watu wenye asili ya Afrika, ambayo huangukia tarehe 31 Agosti.

Siku hii ni siku ya kusherehekea mchango mkubwa ulitolewa na watu wenye asili ya Afrika katika maendeleo ya binadamu. Siku hii imechelewa sana, lakini inaonyesha kutambua kukosa haki na ubaguzi wa kupangwa waliokabiliwa nao watu wenye asili ya Afrika kwa karne nyingi, na wanaendelea kukabiliana nao.

Amekumbusha kutambua madhara ya utumwa, kuondoa dosari zilizotokea kwenye historia, na kukomesha uongo wa umwamba na vitendo vyake vya kila siku, katika kila ngazi na kila jamii. Amesema dunia inatakiwa kukubaliana kuhimiza usawa, haki na heshima kwa wote.