Bunge la Tanzania yatangaza hatua za kuzuia maambukizi ya COVID-19
2021-09-01 10:05:11| CRI

Bunge la Tanzania limetangaza hatua zinazolenga kuzuia maambukizi ya COVID-19 wakati wabunge wakijumuika kufanya mkutano.

Hatua hizo ni pamoja na kupunguza muda wa vikao vya wiki mbili kutoka saa 7 hadi 5 kwa siku. Spika wa bunge Bw. Job Ndugai amesema kwenye ufunguzi wa vikao vya wiki mbili, kwamba mbali na kupunguza muda wabunge wote watatakiwa kuvaa barakoa katika vikao hivyo.

Pia amesema ni wabunge wenye mahitaji maalumu yaliyoidhinishwa na wafanyakazi wa afya wataruhusiwa kuhudhuria vikao bila barakoa.

Ameongeza kuwa kumbi mbili zitatumiwa na wabunge hao ili kuhakikisha umbali wa kijamii, huku akisema wageni wanaotembelea bunge hawataruhusiwa isipokuwa wanahabari wanaoripoti mijadala ya bunge.