Kenya na Pakistan kusaini makubaliano ya kukuza biashara kati yao
2021-09-01 14:57:54| CRI

Kenya na Pakistan zitasaini hati za maelewano (MoUs) kabla ya mwisho wa mwaka huu ili kukuza biashara kati ya nchi hizo mbili.

Waziri wa Viwanda, Biashara na Maendeleo ya Makampuni ya Kenya Bibi Betty Maina amesema makubaliano mawili kuhusu uhifadhi wa miembe na uagizaji wa machungwa kutoka Pakistan yamehitimishwa na yako tayari kusainiwa.

Bibi Maina pia amesema kuwa Kenya imeandaa makubaliano mawili kuhusu uuzaji wa maparachichi na karanga kwa Pakistan kwa ajili ya mapitio na yanatarajiwa kusainiwa mwishoni mwa mwaka huu.  

Pakistan tayari imeondoa ada ya uthibitisho wa hati za uagizaji wa chai kutoka Kenya ili kuhimiza biashara ya bidhaa hiyo.