Madaktari wa China waleta matumaini kwa wagonjwa wa Rwanda katika hospitali ya Masaka
2021-09-02 09:10:31| CRI

Uwepo wa madaktari wa China katika hospitali ya Masaka iliyoko pembezoni mwa mji wa Kigali, Rwanda unaleta mabadiliko kwa huduma za afya nchini Rwanda kupitia kutoa matibabu ya kitaalamu kwa wagonjwa wa Rwanda.

Matie Turinumuremyi mwenye miaka 26 ni mmoja wa wagonjwa wanaopewa matibabu na madaktari wa China katika hospitali hiyo. Amesema anaamini kuwa madaktari wa China watamtibu kwa kuwa mwenzake alipona haraka baada ya kupewa matibabu na madaktari hao.

Mwuguzi mkuu wa kitengo cha upasuaji cha hospitali ya Masaka Aimee Uwiragiye alisema madaktari wa China wameleta mabadiliko makubwa katika hospitali hiyo, hasa kwenye kuboresha huduma za matibabu na utunzaji wa wagonjwa.