Hali ya kibinadamu huko Tigray nchini Ethiopia yazorota
2021-09-02 09:35:46| CRI

Ofisi ya uratibu wa mambo ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa OCHA imesema hali ya kibinadamu huko Tigray nchini Ethiopia inazidi kuzorota, huku wakikaribia kuishiwa na misaada, pesa taslim na mafuta.

OCHA imesema akiba ya chakula ya wadau wa Umoja wa Mataifa imeisha, isipokuwa kwenye maeneo ambayo vifaa tayari vimetumwa. kutokana na kukosekana kwa usalama pamoja na changamoto za urasimu na ugavi, njia pekee ya kufika Tigray kupitia mkoa wa Afar imekuwa haipitiki tangu Agosti 22.

OCHA pia imezitaka pande zote hasimu ziruhusu na kuwezesha usambazaji wa misaada wa kibinadamu kwa watu wote walioathiriwa.