Wanafunzi 73 watekwa nyara kaskazini-magharibi mwa Nigeria
2021-09-02 09:38:51| cri

Polisi wa Nigeria wamesema wanafunzi 73 wametekwa nyara jana asubuhi na watu wenye silaha wasiojulikana kutoka shule moja ya sekondari katika kijiji cha Kaya jimbo la Zamfara, kaskazini-magharibi mwa nchi hiyo.

Msemaji wa Polisi wa jimbo la Zamfara Mohammed Shehu, amesema timu ya utafutaji na uokoaji imetumwa kufanya kazi pamoja na wanajeshi ili kuhakikisha wanawaokoa wanafunzi hao salama, na ulinzi katika kijiji cha Kaya umeimarishwa ili kuzuia matukio zaidi kama hayo kutokea.

Kamishna wa Polisi wa jimbo hilo Ayuba Elkana amesema serikali ya huko imeamuru shule zote za msingi na za sekondari katika jimbo hilo kufungwa baada ya tukio hilo kutokea. Na marufuku ya kutoka nje kuanzia jioni hadi alfajiri imewekwa kwenye sehemu zote 13 za jimbo hilo ili kukabiliana na matukio ya ujambazi na utekaji nyara yanayoongezeka hivi karibuni.