Sudan Kusini kuzalisha oksijeni ili kupambana na COVID-19
2021-09-03 09:56:15| CRI

Sudan Kusini imesema imeanza kuzalisha oksijeni baada ya kiwanda cha kwanza cha kutengeneza oksijeni kuzinduliwa katika Hospitali ya Mafunzo ya Juba.

Waziri wa afya wa Sudan Kusini Bibi Elizabeth Achuei amesema kiwanda hicho kilichoidhinishwa chini ya mpango wa Shirika la Afya Duniani (WHO) na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) kitasaidia nchi hiyo kujiandaa kwa utoaji wa oksijeni ili kukabiliana na wimbi la tatu la maambukizi ya virusi vya Corona.

Wizara hiyo pia imesema kiwanda hicho kinachoweza kuzalisha lita 2,500 za oksijeni na kujaza mitungi 72 ya oksijeni za aina ya D kwa siku, kitakuwa kiini cha uzalishaji na ugavi wa oksijeni kwa maneno ya mbali.