Umoja wa Afrika watoa mafunzo kwa maofisa 27 wa Somalia kulinda usalama wa uchaguzi
2021-09-03 09:41:41| CRI

Tume ya Umoja wa Afrika nchini Somalia AMISOM imesema, maofisa 27 wa polisi wa Somalia wamemaliza mafunzo ya siku tano kuhusu jinsi ya kulinda kwa ufanisi usalama wa uchaguzi unaoendelea nchini humo.

Mafunzo hayo kwa maofisa wa polisi kutoka serikali na majimbo mawili ya Puntland na Galmudug, yanazingatia kujenga uwezo wa washiriki katika utaratibu wa sheria za uchaguzi, michango na majukumu ya kamanda wa polisi na kikosi cha usalama kwenye uchaguzi na usimamizi wa utaratibu wa umma, huku yakitoa mwongozo kuhusu masuala yanayohusiana na usalama wa kijinsia.

Mwezi wa Mei kiongozi wa Somalia alitangaza kuanzisha mchakato wa uchaguzi ndani ya siku 60, ili kupunguza hali ya wasiwasi iliyotokana na rais Mohamed Farmajo kurefusha muda wake madarakani.