Tanzania kuweka mitambo 25 ya kutoa oksijeni kuwasaidia wagonjwa wa COVID-19
2021-09-06 08:31:29| CRI

Mamlaka za afya nchini Tanzania zimesema zimeanza kuweka mitambo 25 ya kutoa oksijeni nchini humo katika juhudi za kuwasaidia wagonjwa wa COVID-19 wanaokabiliwa na tatizo la upumuaji.

Mkurugenzi wa huduma za kuzuia maambukizi katika Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto nchini humo, Bw. Leonard Subi amesema, kila mtambo wa kutoa oksijeni utakuwa na uwezo wa kujaza mitungi 200 ya oksijeni.

Amesema hatua hiyo itaondoa uhaba wa oksijeni wakati kuna ongezeko la watu wanaoambukizwa virusi hivyo wanaopata matatizo ya kupumua.