Somalia yaahirisha tena uchaguzi wa rais na wabunge
2021-09-06 08:30:21| CRI

Tume ya Uchaguzi nchini Somalia (FEC) imeahirisha tena kuanza kwa uchaguzi usio wa moja kwa moja wa rais na wabunge ambao ulipangwa kuanza mwezi huu na mwezi ujao.

Ratiba ya mabadiliko ya tarehe ya uchaguzi iliyotolewa na Tume hiyo jumamosi jioni imesema, uchaguzi unaoendelea sasa wa bunge la juu utaendelea mpaka tarehe 18 mwezi huu, na uchaguzi wa bunge la chini utaanza Oktoba Mosi na kumalizika Novemba 20, hivyo kuchelewesha uchaguzi wa rais uliopangwa kufanyika Oktoba 10.

Tume hiyo haikutoa sababu za kuahirisha uchaguzi wa rais na wabunge, na pia haikutoa tarehe ya kufanyika kwa uchaguzi wa rais ambao unatarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu.