Sudan yakana madai ya Ethiopia kuwa inashirikiana na makundi yenye silaha kulenga Bwawa la Mto Nile
2021-09-06 08:30:55| CRI

Sudan imepinga rasmi kauli iliyotolewa na Ethiopia kuhusu nchi hiyo kushirikiana na makundi ya waasi kutokea ardhi ya Sudan, kufanya mashambulizi dhidi ya Bwawa la GERD.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Sudan imetoa taarifa ikisema, imefuatilia kwa masikitiko makubwa, kauli zisizo za kweli zinazodai kuwa makundi yenye silaha yameingia kwenye mpaka wa Sudan kwa lengo la kufanya mashambulizi dhidi ya Bwawa hilo.

Wizara hiyo imekanusha kauli hizo zisizo na ukweli, na kusisitiza kuwa Sudan inafuata kwa uhalisi kanuni za ujirani mwema na sera ya kutoingilia kati mambo ya ndani ya nchi nyingine.

Ijumaa iliyopita, jeshi la Ethiopia liliripoti kuwa kundi la Harakati za Ukombozi wa Watu wa Tigray (TPLF) lilijaribu kufanya shambulizi dhidi ya Bwawa la GERD na kusababisha vifo na majeruhi.