Xi Jinping autumia barua ya pongezi Mkutano wa 32 wa kimataifa wa sayansi ya usafiri wa anga
2021-09-06 10:50:51| cri

Rais Xi Jinping wa China tarehe 6 ameutumia barua ya pongezi Mkutano wa 32 wa kimataifa wa sayansi ya usafiri wa anga unaofanyika mjini Shanghai, China.

Kwenye barua yake rais Xi amesema sayansi na teknolojia ya usafiri wa anga ni mojawapo ya sekta za kisayansi zinazoendelea kwa kasi na kuleta athari zaidi kwa maisha na shughuli za uzalishaji wa watu tangu kuingia karne ya 20. Mapinduzi ya teknolojia na mabadiliko ya sekta za uzalishaji yametokea kwenye dunia ya sasa, hali ambayo inailetea sayansi na teknolojia ya usafiri wa anga fursa nzuri ya maendeleo. Inahitaji kufanya ushirikiano wa sayansi ya usafiri wa anga duniani, ambao una mustakabali mzuri. Ametaka mkutano huo utoe mchango kwa ajili ya kuhimiza ushirikiano huo na kuwanufaisha zaidi watu wa nchi mbalimbali.