Kundi la waasi la Guinea lamkamata rais wa nchi hiyo
2021-09-06 08:28:25| CRI

Kundi la waasi la Guinea lamkamata rais wa nchi hiyo_fororder_VCG111346703425

Wanajeshi wa kikosi maalumu cha Guinea jana wamemkamata rais Alpha Conde na kuvunja serikali.

Wizara ya ulinzi ya Guinea jana usiku ilitoa taarifa ikisema, kikosi maalumu cha nchi hiyo kimefanya shambulizi karibu na Ikulu, na kusababisha hofu na wasiwasi wa raia, na kuongeza kuwa, kikosi cha ulinzi cha rais na jeshi la serikali vimewaondoa waasi na kufanya operesheni ya msako.

Lakini kikosi maalumu cha jeshi la Guinea kimetangaza kudhibiti madaraka ya nchi na kumkamata rais Conde, kuvunja serikali ya Guinea, na kufunga mipaka ya ardhi ya nchi hiyo kwa wiki moja.

Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika, ECOWAS na mashirika mengine ya kimataifa yamelaani kitendo cha jeshi kuchukua madaraka kwa nguvu na kutaka rais Conde kuawachiliwa haraka iwezekanavyo.