Rais wa China apongeza uzinduzi wa kituo cha kimataifa cha utafiti wa data kubwa kwa ajili ya malengo ya maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa
2021-09-07 13:44:17| cri

Rais Xi Jinping wa China ametoa barua ikipongeza uzinduzi wa kituo cha kimataifa cha utafiti wa data kubwa kwa ajili ya malengo ya maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa.

Kwenye barua hiyo, rais Xi ameeleza kuwa uzinduzi wa kituo hicho ni hatua muhimu ya kutekeleza wito wake alioutoa katika kikao cha 75 cha Umoja wa Mataifa wa kuunga mkono ajenda ya mwaka 2030 ya maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa, ambayo inaweka bayana malengo kwa nchi zinazoendelea pamoja na ushirikiano na maendeleo ya dunia.

Rais Xi pia amesema, dunia inadidimia kutokana na athari zinazoletwa na COVID-19. Uvumbuzi wa sayansi na teknolojia na matumizi ya data kubwa vitasaidia jumuiya ya kimataifa kutatua matatizo na kutekeleza ajenda ya mwaka 2030 ya Umoja wa Mataifa.