Katibu mkuu wa Jubilee asema ripoti ya Marekani kuhusu chanzo cha Virusi vya Corona inatokana na lengo la kisiasa
2021-09-08 08:43:26| CRI

Katibu mkuu wa Jubilee asema ripoti ya Marekani kuhusu chanzo cha Virusi vya Corona inatokana na lengo la kisiasa_fororder_src=http___upload.cbg.cn_2020_0203_1580694812137.png&refer=http___upload.cbg (1)

Katibu mkuu wa chama tawala nchini Kenya, Jubilee, Raphael Tuju amesema, ripoti iliyotolewa na shirika la upelelezi la Marekani kuhusu chanzo cha virusi vya Corona haijafuata msingi wa sayansi, bali ni kutokana na lengo la kisiasa.

Bw. Tuju amesema ripoti hiyo haisaidii kukabiliana na maambukizi ya virusi hiyo na maambukizi mengine yanayowezekana kutokea, na kuongeza kuwa, jumuiya ya kimataifa inapaswa kufanya juhudi katika kukabiliana na janga hilo ili kuwafanya watu wengi zaidi wapate chanjo.

Pia amesema, China imetoa msaada wa chanjo na vifaa vingine kwa nchi nyingine ikiwemo Kenya, na kutoa uzoefu wake wa kupambana na janga hilo.