Jeshi la Guinea latangaza kuunga mkono Kamati ya Kitaifa ya Mshikamano na Maendeleo
2021-09-08 09:13:22| cri

 

 

     Maofisa wa ngazi mbalimbali wa jeshi la Guinea jana wamefanya mazungumzo na kiongozi wa mapinduzi, Luteni Kanali Mamady Doumbouya, ambapo wametangaza kuwaunga mkono wanajeshi walioshiriki kwenye mapinduzi ya kisiasa na Kamati ya Kitaifa ya Mshikamano na Maendeleo iliyoundwa na waasi hao.

    Katika mazungumzo hayo, Wizara ya ulinzi ya Guinea imesema, ili kulinda maslahi ya taifa na kuzuia uvamizi kutoka nje, jeshi la nchi hiyo limeamua kuwaunga mkono wanajeshi walioshiriki kwenye mapinduzi hayo, na kusema jeshi hilo litaendelea kulinda amani na utulivu nchini humo.