Umoja wa Afrika kuisaidia Somalia kufanya uchaguzi wa kuaminika
2021-09-08 08:55:06| cri

Umoja wa Afrika kuisaidia Somalia kufanya uchaguzi wa kuaminika_fororder_AU

Kamati ya Umoja wa Afrika kwa kushirikiana na Ujumbe wa Umoja humo nchini Somalia (AMISOM) imeanza kusaidia mchakato wa uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika baadaye mwaka huu.

Umoja huo umesema, msaada huo ni pamoja na msaada wa kifedha, kiutendaji, na wa kiufundi, kutokana na ombi lililotolewa na serikali ya Somalia.

AMISOM imesema misaada hiyo itachangia kufanikiwa kwa uchaguzi huo ambao ni msingi thabiti wa juhudi zinazoendelea za kutimiza demokrasia, amani na utulivu wa kisiasa nchini Somalia.