Mafanikio ya CPC yatokana na sera yake ya kuweka wananchi kwanza
2021-09-09 09:47:55| CRI

Msomi wa Tanzania asema mafanikio ya CPC yatokana na sera yake ya kuweka wananchi kwanza_fororder_TZ

Profesa Humphrey Moshi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salam amesema, mafanikio makubwa ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) ambacho mwaka huu kimetimiza miaka 100 tangu kuanzishwa, yanatokana na sera yake ya kuweka wananchi kwanza.

Profesa Moshi amesema, CPC imeweza kudumu na kupata mafanikio makubwa katika kipindi hicho cha miaka 100 kutokana na kuweka wananchi wake kwanza na kuwaletea maendeleo. Amesema uongozi wa Chama ambao umeleta maendeleo ni uongozi wenye sifa kuu tatu, ambazo amezitaja kuwa ni dira ya muda mrefu, viongozi kupenda maendeleo ya wananchi wanaowaongoza, na ukaribu kati ya viongozi na wananchi katika nyanja mbalimbali.