Waziri wa mambo ya nje wa Zimbabwe asisitiza utafutaji wa chanzo cha COVID-19 unatakiwa kufanyika kwa njia ya kisayansi
2021-09-09 10:41:43| cri

Kwa mujibu wa Tovuti ya New Zimbabwe, waziri wa mambo ya nje wa Zimbabwe Frederick Shava amesema hivi karibuni kuwa watu wanapaswa kuamini sayansi na kuheshimu maoni ya wataalamu wa Shirika la Afya Duniani. Ripoti ya uchunguzi wa pamoja ya kutafuta chanzo cha virusi vya Corona imeonyesha kuwa hakuna uwezekano kwamba virusi hivyo vilisambaa baada ya kuvuja katika maabara na haifai kuiacha China ibebe lawama kuhusu janga hilo.