Umoja wa Mataifa waahidi kupambana na ugaidi katika kumbukumbu ya mashambulizi ya tarehe 11 mwezi Septemba
2021-09-10 10:32:58| cri

 

 

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa jana limeahidi kupambana na ugaidi miaka 20 baaada ya mashambulizi yaliyotokea tarehe 11 mwezi Septemba nchini Marekani.

 Taarifa iliyotolewa na Baraza hilo imesema, nchi wajumbe wa Baraza hilo hivi sasa wanashikamana kama walivyokuwa miaka 20 iliyopita, na watafanya juhudi kuzuia na kupambana na ugaidi wa aina yoyote na sehemu yoyote kwa mujibu wa sheria ya kimataifa.

Taarifa hiyo pia imesema, nchi hizo wajumbe zimetoa salamu za rambirambi kwa ndugu na marafiki wa watu waliouawa kwenye mashambulizi hayo, ambapo zaidi ya nchi 90 zilipoteza raia wao.