Waziri mkuu wa China azihimiza nchi za eneo kuu la Mekong GMS kupanua ushirikiano
2021-09-10 11:53:13| cri

Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang ametoa wito wa kupanua sekta za ushirikiano kati ya nchi za eneo kuu la Mekong GMS na kuhimiza kwa pamoja maendeleo endelevu na jumuishi katika kanda hiyo.

Bw. Li amesema hayo kwenye Mkutano wa 7 wa kilele wa ushirikiano wa kiuchumi wa GMS, ambao uliongozwa na mwenzake wa Cambodia Samdech Techo Hun Sen.

Bw. Li amesema, wakati maambukizi ya COVID-19 yakiendelea kote dunaini, mambo yasiyo na uhakika katika uchumi wa dunia yanaongezeka, na kuongeza kuwa ufufukaji na uendelevu wa uchumi wa nchi za GMS unakabiliwa na changamoto mpya.

Amesisitiza kuwa inapaswa kujenga maoni ya pamoja, kuimarisha maelewano ya kisiasa, kupanua maeneo ya ushirikiano, kuzidisha kiwango cha ushirikiano na kuhimiza kwa pamoja maendeleo endelevu na jumuishi katika kanda hiyo.