ECOWAS yasimamisha uanachama wa Guinea
2021-09-10 10:28:06| cri

Nchi wanachama wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) zimefanya mkutano maalum kupitia mtandao na kuamua kusitisha uanachama wa Guinea.

Baada ya mkutano huo, ECOWAS ilitoa taarifa ikilaani mapinduzi ya kisiasa yaliyofanyika nchini Guinea, na kupinga vikali mapinduzi yoyote ya kisiasa yanayokiuka katiba. Jumuiya hiyo imewataka wanajeshi waliohusika na mapinduzi hayo kulinda usalama wa rais Alfa Conte wa nchi hiyo, na kumwachia mara moja rais huyo bila masharti pamoja na watu wengine wanaoshikiliwa na wanajeshi hao.

Taarifa hiyo pia imesema, ujumbe wa ECOWAS umekwenda Guinea jana kukutana na wanajeshi hao.