Uchumi wa Kenya kuongezeka kwa zaidi ya 6% mwaka huu
2021-09-10 08:34:52| CRI

Uchumi wa Kenya kuongezeka kwa zaidi ya 6% mwaka huu_fororder_VCG111338666644

Uchumi wa Kenya unatabiriwa kuongezeka kwa zaidi ya asilimia 6 mwaka huu baada ya kupungua kwa asilimia 0.3 katika mwaka 2020 kutokana na athari ya maambukizi ya COVID-19.

Waziri wa Fedha na Mipango nchini humo Ukur Yatani amesema hayo jana, na kuongeza kuwa, ongezeko la uchumi duniani litaongeza mahitaji ya bidhaa za Kenya katika nchi za nje na kuhimiza ongezeko la uchumi la nchi hiyo.

Bw. Ukur aliyasema hayo alipotoa ripoti ya uchumi wa Kenya ya mwaka 2021 iliyotolewa na Idara ya Takwimu ya Kenya.