Viongozi wa Somalia wahimizwa kuepusha mgogoro wa kisiasa na kuleta utulivu
2021-09-13 09:26:10| cri

Naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Amina J. Mohammed ametoa wito kwa viongozi wa kisiasa wa Somalia kuepusha mgogoro wa kisiasa unaoweza kuharibu maendeleo yaliyopatikana nchini humo.

Akiwa kwenye ziara ya siku moja mjini Mogadishu na kukutana na rais Mohamed Farmajo na waziri mkuu Mohamed Roble, Mohammed alisema Somalia imepata maendeleo ya kutia moyo kwa kushuhudia mchakato unaoendelea wa uchaguzi mkuu, na viongozi hawa wanapaswa kupunguza mvutano wa kisiasa nchini humo.

Somalia hivi sasa inafanya uchaguzi wa seneti na kufanya maandalizi kwa ajili ya uchaguzi wa baraza la wawakilishi.