Katibu mkuu wa UM atoa wito wa kuimarisha ushirikiano wa kimataifa ili kukabiliana na changamoto ya afya duniani
2021-09-13 09:25:20| cri

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres ametoa wito wa kuimarisha ushirikiano wa kimataifa ili kukabiliana na changamoto ya afya duniani, na kupunguza umaskini na ukosefu wa usawa.

Bw. Guterres amesema hayo katika ujumbe wake wa video kwa ajili ya Siku ya Umoja wa Mataifa ya Ushirikiano ya Kusini-Kusini, ambayo inasherehekewa duniani tarehe 12 Septemba kila mwaka.

Ametoa wito wa kujenga jamii shirikishi na yenye ustahimilivu, kuwawezesha wanawake na vijana, kutumia teknolojia ya dijitali, na kupanua mipango endelevu ya fedha.

Pia amesema ushirikiano wa Kusini-Kusini na wa pande tatu umetoa ufumbuzi kwa changamoto hizo za pamoja, na Umoja wa Mataifa utaendelea kuunga mkono juhudi hizo.