Misri yafungua Maonyesho ya 33 ya Kilimo ya Afrika na Mashariki ya Kati
2021-09-13 09:24:42| cri

Misri jana Jumapili ilifungua Maonyesho ya 33 ya Sahara, ambayo pia ni Maonyesho ya Kilimo ya Kimataifa kwa Afrika na Mashariki ya Kati, katika Kituo cha Maonyesho cha Kimataifa cha Misri.

Chini ya usimamizi wa Wizara ya Utamaduni na Ukombozi wa Ardhi ya Misri, maonyesho hayo ya siku nne yanadhaminiwa na benki kadhaa za kitaifa za Misri na wawekezaji, yakikusanya washiriki wa maonesho hayo kutoka Misri, China, Russia, Italia, Uholanzi, Jordan na Lebanon.

Waziri wa Kilimo wa Misri Bw. El-Sayed el-Quseir amesema kuwa dunia nzima imeanza kuzingatia sekta ya kilimo kwa sababu ya imani katika umuhimu wake haswa wakati wa janga la COVID-19, na kuongeza kuwa sekta hiyo ni rahisi kubadilika na kuondoa athari kwa kiwango cha ukuaji wa haraka.