Korea Kaskazini yafanya jaribio la aina mpya ya makombora ya masafa marefu
2021-09-13 09:24:19| cri

Korea Kaskazini yafanya jaribio la aina mpya ya makombora ya masafa marefu_fororder_NK

Shirika la Habari la Korea (KCNA) limeripoti kuwa nchi hiyo imefanikiwa kujaribu aina mpya ya makombora ya masafa marefu siku ya Jumamosi na Jumapili.

Makombora ya masafa marefu yaliyorushwa yalisafiri kwa sekunde 7,580 juu ya anga ya ardhi ya eneo na bahari ya Korea Kaskazini na kupiga shabaha iliyopo umbali wa kilomita 1,500 .

Habari zimesema kuwa mfumo huu wa silaha unashikilia umuhimu wa kimkakati wa kumiliki njia nyingine nzuri ya kuzuia ambayo inahakikisha usalama zaidi wa nchi hiyo na kudhibiti vikali operesheni za kijeshi za vikosi vyenye uadui na nchi hiyo.