Afrika Kusini yalegeza masharti ya zuio kuanzia Jumatatu
2021-09-13 09:23:08| cri

Afrika Kusini yalegeza masharti ya zuio kuanzia Jumatatu_fororder_SA

Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini jana alitangaza kuwa kuanzia leo Jumatatu Afrika Kusini itapunguza kiwango cha tahadhari kutoka cha tatu hadi cha pili.

Amesema ingawa awamu ya tatu ya janga la Corona bado haijamalizika, lakini idadi ya watu wanaoambukizwa imepungua katika wiki kadhaa zilizopita, ambapo idadi ya wastani ya maambukizi ya kila siku kwa wiki iliyopita ilikuwa asilimia 29 ikiwa chini kuliko siku 7 za nyuma, na chini kwa asilimia 48 kuliko siku 7 kabla ya hapo. Kwa tangazo hilo sasa muda wa marufuku ya kutoka nje usiku utaanzia saa tano usiku hadi saa kumi alfajiri, mikusanyiko yote ya ndani haitazidi watu 250, na ya nje haitazidi 500.

Ameongeza kuwa serikali itatoa taarifa zaidi kuhusu njia ya kutoa viza ya paspoti ambayo itatumika kama kitambulisho cha kuonesha kwamba umepewa chanjo ya Corona.