Mtanzania mmoja akamatwa kwa kusafirisha wahamiaji 16 wa Ethiopia
2021-09-14 09:13:49| cri

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Mbeya, nchini Tanzania Bw. Ulrich Matei ametangaza kuwa polisi wamemkamata raia mmoja wa Tanzania akihusishwa na usafirishaji wa wahamiaji haramu 16 wa Ethiopia, na kuongeza kuwa mtuhumiwa huyo ni Yohana Adam, mkazi wa Kasumulu katika wilaya ya Kyela mkoani Mbeya.

Matei amesema kuwa mtuhumiwa huyo alikamatwa Jumapili jioni wakati aliposafirisha wahamiaji hao haramu kwenda Afrika Kusini kupitia nchi jirani ya Malawi. Waethiopia hao walisafirishwa kwenye gari lililoendeshwa na mshukiwa, na wengi wao ni vijana wenye umri kati ya miaka 11 na 18.

Aidha polisi pia wanawasaka washukiwa wengine sita ambao wanadaiwa kuendesha kundi la biashara ya binadamu katika mkoa huo.