Kenya Airways yasaini mkataba wa kukodisha ndege na kutumia nambari za siri pamoja na Shirika la Ndege la DRC
2021-09-14 09:13:24| cri

Shirika la Ndege la Kenya limesaini makubaliano ya kukodisha ndege na kuanza kutumia pamoja nambari za mizigo na Shirika la Ndege la Kongo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege la Kenya Bw. Allan Kilavuka, alisema kuwa ushirikiano huo unaimarisha uhusiano wa anga kati ya Kenya na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), na kutekeleza makubaliano kati ya kampuni hizo mbili yaliyosainiwa mwezi Aprili.

Ameongeza kuwa makubaliano hayo yatashuhudia Shirika la Ndege la Kenya likikodisha ndege mbili za Embraer E190 kwa Shirika la Ndege la DRC, na kupiga jeki shughuli za ndani na safari za ndege nchini DRC.

Anaona kuwa ushirikiano huo ni hatua ya kwanza kati ya hatua nyingi katika kufanikisha jamii ya kiafrika kwa kuunda mfano wa ushirikiano kati ya mashirika mawili ya ndege ya Afrika, ambayo yatachangia maendeleo ya kijamii na kiuchumi ya Afrika.

Shirika la Ndege la Kenya pia lilitangaza kuanza safari za moja kwa moja za ndege za mizigo kutoka Johannesburg Afrika Kusini kwenda Lubumbashi nchini DRC.