Wafungwa 240 watoroka baada ya mtu mwenye silaha kushambulia gereza nchini Nigeria
2021-09-14 09:12:41| cri

Serikali ya Nigeria imesema msako wa kuwatafuta wafungwa 240 waliotoroka umeanza baada ya mtu mwenye silaha asiyejulikana kushambulia gereza lililopo mji wa Kabba jimboni Kogi.

Msemaji wa gereza hilo (NCoS) Francis Enobore amesema kwenye taarifa kwamba washambuliaji walivunja na kuvamia kituo hicho Jumapili usiku baada ya mapambano ya kurushiana risasi na walinzi, na kulazimisha kuachiliwa karibu wafungwa 240. Enobore amefafanua kuwa NCoS imeanza utaratibu wa kuwakamata na kuwaomba wenyeji wa huko kusaidia askari wa usalama kwa kuwapa taarifa muhimu ambazo zitasaidia kukamatwa kwa wafungwa hao walitoroka.

Hadi wakati shambulizi linatokea gereza hilo lilikuwa na wafungwa 294 ambapo kati yao 224 wamezuiwa wakiendelea na kesi zao na 70 wameshahukumiwa kifungo.