Uchumi wa Tanzania wakua kwa asilimia 4.9 katika robo ya kwanza ya mwaka huu
2021-09-15 09:26:42| cri

Benki kuu ya Tanzania (BOT) imetangaza kuwa uchumi wa nchi hiyo umekua kwa asilimia 4.9 katika robo ya kwanza ya mwaka 2021 ambayo ni ndogo ikilinganishwa na asilimia 5.9 iliyorekodiwa mwaka 2020 kipindi kama hiki.

Kwenye taarifa yake iliyotolewa baada ya kamati yake ya sera ya fedha kukutana Septemba, 13 na kukagua mwenendo wa sera ya fedha na utendaji wa kiuchumi katika siku za hivi karibuni na mtazamo wa jumla wa uchumi, BOT imesema ukuaji huo ulichochewa na shughuli za ujenzi, uchukuzi, kilimo, viwanda, madini na uchimbaji wa mawe.

Kulingana na taarifa hiyo, uchumi unatarajiwa kuendelea kuimarika, kwa sababu ya uwekezaji wa umma unaoendelea na uchumi wa dunia kurejea hali ya kawaida, mambo ambayo yatafanya uwekezaji wa sekta binafsi na biashara kuongezeka.

Aidha utendaji wa sekta ya nje ya uchumi unaendelea kukabiliwa na changamoto zinazosababishwa na COVID-19, haswa utalii.