Mapigano mapya kati ya vikundi vya upinzani vya Sudan Kusini yasababisha vifo vya watu zaidi ya 20
2021-09-15 09:27:13| cri

Msemaji wa SPLA-IO aliye chini ya Makamu wa Rais wa kwanza wa Sudan Kusini Riek Machar Bw. Lam Paul Gabriel amesema kuwa wakuu watatu wa jeshi pamoja na wanajeshi zaidi ya 20 waliuawa katika mapigano mapya yaliyozuka Jumatatu kati ya vikundi hasimu vya kundi la upinzani la Sudan Kusini ambalo ni Jumuiya ya Ukombozi wa Watu wa Sudan na Upinzani wa Jeshi (SPLM na A-IO) huko Morjala na eneo la Gazal la jimbo la Upper Nile.

Mapigano hayo mapya yalitokea baada ya kikundi kilichojitenga cha SPLM / A-IO kinachoongozwa na mnadhimu mkuu wa zamani wa Machar, Simon Gatwech Dual mnamo tarehe 4 mwezi Agosti  kupambana huko Magenis na wanajeshi watiifu, na kupelekea wanajeshi 34 kuuawa.